SAIDIA GONGO LA MBOTO -United Kingdom
Gongo la Mboto Fundraising uk
Ndugu zangu na marafiki zangu wapenzi kama mnavyo jua wiki hii kuna janga kubwa sana limetokea huko nyumbani Tanzania na maisha ya watu wengi sana yako mashakani. Watu hawana makazi, watoto wamepotea, wengine wako mahospitalini na hali ya kiuchumi pia ni utata. Nimefikiria na wenzangu tukaona tuanzishe kitu kinaitwa "SAIDIA GONGO LA MBOTO". Kwa wale marafiki zetu mliopo UK au popote pale na mtapenda kuchangia tumeona ni bora tukachangia chochote tulicho nacho and then tuwakilishe Ubalozini na majina ya wale wote tuliojitolea chochote ili ubalozi utusaidie kuwakilisha mchango wetu na kutupatia report ni wapi huo msaada umekwenda na kama ni pesa zimefanya kitu gani kwa ajili ya watu hao. Haijalishi ni kiasi gani cha pesa au kitu gani utatoa, utoe tu kutokana na uwezo ulio nao 'it will still make a difference to the people out there'. Msaada unahitajika haraka iwezekanavyo. Ukihitaji receipt pia utapata.
KWA WAKAZI WA LONDON NA MIJI YA KARIBU AU KAMA UTA WEZA KUFIKA TUTAKUWA:
AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT
81 BROAD LANE
SEVEN SISTERS
LONDON
NW15 4DW
SIKU: JUMAPILI TAREHE 27 FEB 2011
MUDA: 3PM - LATE
KWA WAKAZI WA READING NA MIJI YA KARIBU AU KAMA UTA WEZA KUFIKA TUTAKUWA:
VINCENT RESTAURANT
288-290
OXFORD ROAD
READING
SIKU: JUMAMOSI 26 FEBRUARY 2011
MUDA: 3PM - LATE
TAFADHALI LETA CHOCHOTE ULICHO NACHO ILI TUWEZE KUWASAIDIA HAWA NDUGU ZETU WALIO PATWA NA MAAFA HUKO NYUMBANI TANZANIA
KWA WAKAZI WA MIJI MINGINE AMBAO MTASHINDWA KUFIKA LONDON TUNAPANGA UTARATIBU WA JINISI GANI TUNAWEZA KUFIKA KATIKA MIJI YENU KUKUSANYA HIYO MISAADA. TUTAWAJULISHA MARA MIPANGO HII ITAKAPO KAMILIKA.
AU KAMA UNA CHOCHOTE UNAWEZA PIA UKAWEKA KWENYE ACCOUNT IFUATAYO NA TUNAOMBA UANDIKE JINA LAKO AS REFERENCE ILI TUJUE PESA IMETOKA KWA NANI AND CAN BE ACCOUNTED FOR!!
BANK: BARCLAYS
NAME: MISS SHILLA GABRIEL FRISCH
ACCOUNT NUMBER: 40974382
SORT CODE: 202941
FOR MORE INFORMATION YOU CAN REACH US ON
+447527190239 ,
+447404332910 ,
+447876126862 ,
+4407747129987 ,
+447944473389
TAFADHALI MJULISHE NA MWENZIO.
ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI
"SAIDIA GONGO LA MBOTO"
Fat-hya .H. Chambo
Saturday, February 19, 2011

Anna Clara Masala: Muziki wa Injili ni kazi ya Mungu, si umaarufu
Leo katika TGM nakuletea muimbaji wa muziki wa Injili, Anna Masala ambaye ni miongoni mwa waimbaji wa muziki huo nchini Tanzania ambaye ameamua kuimba nyimbo za kumsifu Mungu tangu mwaka 1997 mara baada ya kupata nafasi ya kumpokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.
“Pamoja na ukweli huo lakini nikwambie jambo moja ambalo mimi ninaliona kuwa si sahihi nalo ni ushirikiano mdogo na kukosekana upendo wa dhati miongoni mwetu sisi waimbaji wa muziki wa Injili,” anasema Anna.
Akizungumzia juu ya mwanzo wa huduma yake, Anna anasema kwamba kazi ya uimbaji alianza kuifanya akiwa muimbaji wa kwaya ya kanisani alipokuwa anaabudu, (Tanzania Assemblies of God -TAG-Kinondoni) ambapo kupitia muziki huo, Mungu ameweza kumsimamia kwenye masuala mengi ya kimaendeleo.
Miongoni mwa mambo ambayo anaamini kuwa yametokana na matunda ya kufanya kazi ya kuhubiri Injili kwa njia ya nyimbo, ni pamoja na kupata kazi za kucheza filamu tatu ambazo ni Hero of Church, Kiapo na Danger Zone jambo analoamini kuwa ni kutokana na rehema za Mungu tu.
“Haya kwangu nayaona kuwa ni mafanikio makubwa, lakini haikuwa ni safari nyepesi kwa sababu nilikutana na vikwazo vingi katika maisha yangu, hii si mimi pekee bali waimbaji wengi hukabiliana na mambo haya.
“Pamoja na hayo, pia muziki huu umekuwa ukitumika kwa ajili ya kubadilisha tabia na miondoko ya wanajamii na kumtangaza Mungu, lakini cha kushangaza wapo baadhi ya waimbaji hawapendani, jambo ambalo ni baya kwa mustakabali wa huduma hii,” anaongeza muimbaji huyo ambaye bado hajapata jina kubwa ikilingansihwa na waimbaji wengine waliopo juu hivi sasa kama Rose Mhando, Bahati Bukuku na Upendo Nkone.
Akielezea ushirikiano uliokuwepo baina ya waimbaji chipukizi, anasema kuwa kila wakati wamekuwa wakipeana moyo na kuamini kuwa kufanya muziki wa Injili si kwa ajili ya kutafuta fedha, au umaarufu bali ni kazi ya wito ili kuwaokoa watu wa Mungu na matatizo ya kidunia.
“Japokuwa ni kazi ya Mungu lakini kuna tatizo lingine kubwa nalo ni usumbufu kwenye studio wakati tukijiandaa kurekodi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba studio hizihizi ndizo zinazotumika kurekodi nyimbo za kidunia,” anaongeza mwanadada huyo aliyejikita vilivyo kwenye imani ya kilolole.
Aneleza kuwa studio nyingi za kidunia zinakuwa na matatizo ya kuiba kazi za waimbaji na kuziuza kinyemela huku akikiri kuwa hata yeye alitokewa na jambo hilo.
“Nimalizie kwa kusema kuwa huduma ya uimbaji wa nyimbo za Injili inagusa zaidi kumtumikia Mungu na siyo kujulikana kama baadhi ya watu wanavyodhani, na wakati huo huo niwape moyo watumishi wa Mungu kutokana na kujituma kwao kwenye huduma hii,” anamaliza Anna
Dk. Slaa apinga matokeo
*Asema Usalama wa Taifa wamechakachua kura
*Aeleza tofauti ya zinazotangazwa na za vituoni
*Sasa aiomba jumuiya ya kimataifa iingilie kati
*Ridhiwan asema ameshaona dalili za kushindwa
Na Maregesi Paul
MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, ametoa tuhuma nzito za wizi wa kura akiihusisha Idara ya Usalama wa Taifa.
Amesema kuwa kitendo cha Idara hiyo kujiingiza katika siasa na kushiriki kubadili matokeo ya kura katika maeneo mbalimbali nchini ni cha hatari kwa kuwa viongozi wanaopatikana sio chaguo la wananchi.
Amesema kwamba kubadili matokeo kunaweza kuzua vurugu kwa kuwa wapigakura wanajua ukweli juu ya kinachofanywa.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam, jana.
*Aeleza tofauti ya zinazotangazwa na za vituoni

*Sasa aiomba jumuiya ya kimataifa iingilie kati
*Ridhiwan asema ameshaona dalili za kushindwa
Na Maregesi Paul
MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, ametoa tuhuma nzito za wizi wa kura akiihusisha Idara ya Usalama wa Taifa.
Amesema kuwa kitendo cha Idara hiyo kujiingiza katika siasa na kushiriki kubadili matokeo ya kura katika maeneo mbalimbali nchini ni cha hatari kwa kuwa viongozi wanaopatikana sio chaguo la wananchi.
Amesema kwamba kubadili matokeo kunaweza kuzua vurugu kwa kuwa wapigakura wanajua ukweli juu ya kinachofanywa.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam, jana.
Kama ni urafiki mhh! "hii too much".

Kwa jamii yetu mnyama mbwa anafugwa kwa madhumuni ya kusaidia ulinzi. Ila katika jamii nyingine mnyama huyu ni rafiki mkubwa wa binadamu na anapewa heshima zote za rafiki wa kweli. Kudhihirisha hilo ni kosa kubwa kwa wenzetu hawa kumtaja mnyama huyu kwa kutumia pronoun "it". Huwakilishwa napronoun sawia kabisa na binadamu. Mathalani mbwa dume ni "he" na mbwa jike ni "she". Huo ni mfano mmoja tu wa heshima apewayo mnyama mbwa. Naamini ipo mingi.
Subscribe to:
Comments (Atom)

